1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bosi wa Bayern aiunga mkono Dortmund kuhusu Auba

Sekione Kitojo
19 Januari 2018

Kocha  Jupp Heynckes wa Bayern ameunga mkono uamuzi wa Borussia Dortmund kumwacha mchezaji wao nyota Pierre-Emerick Aubameyang.

https://p.dw.com/p/2rADT
FC Bayern München, Trainer Jupp Heynckes
Picha: picture-alliance/Citypress24

Aubameyang  kwa  mara  nyingine  tena  ameenguliwa  katika  kikosi  cha  Dortmund  katika mchezo  wa  leo  Ijumaa  wa  ligi  dhidi  ya  Hertha  Berlin  baada  ya  pia  kusitishwa  kucheza na  kocha  mkuu  wa  Borussia  Peter Stoeger  katika  mchezo  uliokwenda  suluhu nyumbani dhidi  ya  Wolfsburg.

Mchezaji  huyo  nyota  wa  Borussia  Dortmund  mwenye  umri  wa  miaka 28  amepachika wafuni  mabao 13  katika  michezo  15  ya  ligi  msimu  huu, akifunga  mara  21  katika michezo 23  katika  mashindano  yote.

Jupp Heynckes
Kocha mkuu wa timu ya Bayern Munich Jupp HeynckesPicha: picture-alliance/sampics/S. Matzke

Hata  hivyo , alipewa  karipio  la  utovu  wa  nidhamu  kwa  mara  ya  tatu  katika  muda  wa miezi  16 kwa  kushindwa  kuhudhuria  mkutano  wa  timu  mwishoni  mwa  juma  lililopita.

Baba  yake  mzazi  na  ambaye  ni  wakala  wake anaripotiwa  kuwapo  mjini London akijaribu  kutayarisha  hatua  za  uhamaji  kwenda  Arsenal  kwa  kijana  wake, lakini Heynckes  amesema  Dortmund wako  sahihi  kwa  kumuacha  mfungaji  wao  huyo  nyota.

Aubameyang hatabiriki

Kocha  huyo  wa  Bayern  mwenye  umri  wa  miaka  72  amesema  anasikitishwa  sana hususan baada  ya  Ousmane Dembele kususia  mazowezi  ya  timu Agosti  mwaka  jana katika  juhudi  za  kuilazimisha  Dortmund  kumuuza  kwa  Barcelona.

"Kitu  kinachotokea Dortmund  kuhusu  Dembele  na  Aubameyang unahitaji kukiangalia  kwa undani  zaidi," Heynckes  alisema  mjini  Munich leo Ijumaa(19.01.2018)

Fußball Training Borussia Dortmund AUBAMEYANG
Mshambuliaji nyota wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick AubameyangPicha: picture-alliance/dpa/Revierfoto

"Nafikiri kwamba  klabu  yoyote  inapaswa  kufikiri mara  mbili  juu  ya  kumchukua  mchezaji kama  huyo  na  naweza  kusema kwa  kweli, sitamkubali  mchezaji  kama  huyo.

"Bado  ni  mchezo  wa  timu  nzima na  hakuna  nafasi kwa  hayo.

"Ni  lazima  tuwe waangalifu  kwamba  mashabiki  hawatukimbii katika  wakati  fulani."

Heynckes  amesema  hawezi  kufikiria hali  kama  hiyo  inayoweza  kumhusu  mmoja  kati  ya wachezaji  wake  katika  Bayern.

"Huwezi  kusema  haitaweza  kutokea Bayern , lakini  nasema  wazi  kabisa  siwezi  kufikiria kitu  kama  hivyo  kutokea.

"Wachezaji  wana  wajibu  wao, wana  wajibu  mkubwa kwa  klabu  zao, kwa  hiyo  haitoshi tu kuangalia salio lako  katika  benki mwishoni  mwa   mwezi."

Fußball Dortmunds Trainer Peter Stöger
Kocha wa Borussia Dortmund Peter StoegerPicha: picture-alliance/dpa/T. Frey

Dortmund  iko  nafasi  ya  nne  katika  msimamo  wa  ligi wakati  Bayern inaanza  michezo wa  mwishoni  mwa  juma  ikiwa  na  pointi 13  zaidi  ya  timu  iliyoko  karibu  yake  RB Leipzig  kabla  ya  pambano  la  siku  ya  Jumapili  nyumbaji  dhidi  ya  Werder Bremen.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe