1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOSTON: Wito kwa Marekani kuondoka Irak

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIC

Waziri Mkuu wa Uingereza Dominique de Villepin,ameihimiza Marekani kuondoka Irak ifikapo mwaka 2008,akisema vita vya Irak vimeathiri vibaya sifa ya Marekani.Alipokitembelea chuo kikuu cha Harvard karibu na Boston,Villepin alisema,vita hivyo vimeathiri nchi za Magharibi kwa jumla. Wakati huo huo akasema,Marekani na nchi za Ulaya zinapaswa kuchukua hatua za pamoja ili zipate kuheshimiwa tena na watu wengi,hasa katika nchi za Mashariki ya Kati.Matumizi ya nguvu tu si jawabu aliongezea waziri mkuu wa Ufaransa Villepin.