1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Botswana yapata rais mpya baada kustaafu kwa rais Festus Mogae wa nchi hiyo.

Scholastica Mazula31 Machi 2008

Aliyekuwa Makamu wa rais wa Botswana Seretse Khama Lan Khama, amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/DY1E
Rais mstaafu wa Botswana Festus Mogae katikati akiwa na marais wengine Armando E. Guebuza, na Koehler, 4. Nov. 2007Picha: AP

Wachambuzi wa masuala ya Kisiasa nchini humo wanatarajia kuwa rais huyo mpya ataweza kuendeleza uchumi na siasa za nchi hiyo ambayo imekuwa moja ya nchi zenye historia ya mafaniko barani Afrika.

kuchaguliwa kwa Rais Seretse Khama Lan Khama, kunafuatia kustaafu kwa rais Festus Mogae ambaye amestaafu baada ya kuwa madarakani kwa karibu muongo mzima.

Rais Msitaafu Festus Mogae amemkabidhi madaraka Khama Lan Khama mtoto wa aliyekuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo baada ya Uhuru katika sherehe maalumu zilizofanyika jumanne wiki iliyopita.

Wakati Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo unatarajiwa kufanyika mwaka 2009, Khama mwenye umri wa miaka hamsini na tano atakuwa amerithi uongozi wa kuiongoza moja ya nchi yenye Uchumi imara barani Afrika.

Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini, ambalo ni mzalishaji mkuu wa almasi na maarufu kwa kuwa na mbunga nyingi za wanyama wa pori limekuwa likifurahia kuongezeka kwa uchumi wake hadi asilimia nane katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Banki ya uwekezaji ya dunia, Pato la jumla la nchi hiyo katika masuala ya utalii linafikia dola elfu nane na mianne hamsini na tatu kwa mwaka huu kiwango ambacho ni kikubwa zaidi katika nchi zilizoko Kusini mwa jangwa la sahara.

Mwaka 1999, rais msitaafu Festus Mogae alifanikiwa kumshinda rais Ketumile Masire katika uchaguzi alioshinda kwa kura nyingi kwenye chama Kikuu cha Botswana Democratic -BDP, ambacho kimekuwa madarakani tangu koloni hilo la Uingereza lilipopata Uhuru wake mwaka 1966.

Matarajio makubwa ya raia wa Botswana nikuona kuwa ni nani ataiongoza nchi hiyo yenye watu wapatao milioni mbili.

Skauti mmoja anayefanya kazi katika hifadhi ya wanyama karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Gaboron,(Khaburun) B.Kasome mwenye umri wa miaka 35, anasema kwa upande wake anadhani kila kitu kitabakia kawaida kwa kuwa viongozi wote hao wanatokea katika chama kimoja.

Anasema kwa sasa hawana matatizo na bado wanampenda Mogae na hivyo haoni umuhimu wa wao kubadilisha uongozi ama chama wakati kila kitu kiko sawa.

Wachambuzi wanasema makabidhiano hayo ya madaraka yalifanyika kwa umakini zaidi ili kuzuia kusitokee hali ya machafuko ambayo yamekuwa yakitokea katika sehemu nyingine za bara la Afrika.

Chama tawala cha BDP, ambacho kimekuwa kikishinda katika uchaguzi tangu nchi hiyo ijipatie Uhuru wake kinaonyesha dalili za ushindi hata katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Seretse Khama, ambaye anatokea kwenye jamii ya Kifalme ya watu wa kabila kubwa nchini humo la Bangwato anapewa nafasi kubwa ya ushindi katika uchaguzi huo.

Seretse Khama, ambaye kitaaluma ni Rubani, amekuwa akipendwa na watu wengi nchini humo lakini wengine wamekuwa na hofu kutokana na historia yake ya kijeshi kwamba huenda akaitumia katika utawala wake.

Tshego Ngeza, mwalimu mkuu katika shule moja ya chekechea anasema angependa sana Rais Mogae akaendelea kuwa madarakani kwa sababu watu wengi wanahofia Historia ya nyuma ya rais wa sasa Khama Lan Khama.

Wakati huohuo, mbali na nchi hiyo kusifika kwa uchumi mzuri Serikali ya Botswana imeweza kushinda kwa kiwango kikubwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI duniani.

Kufuatia ushindi huo imepata msaada wa dawa na vitu vingine ili kuweza kuzuia ugonjwa huo ambao unakadiliwa kwamba mmoja kati ya kila watu ameambukizwa.

Botswana imebakia kuwa kisiwa cha amani na baadhi ya raia wake wanaamini kuwa Seretse Khama ni mgombea atakayeweza kuiongoza vyema nchi hiyo.