1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOUAKE : Viongozi wa Afrika kushajiisha amani

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeJ

Viongozi wanane wa mataifa ya Afrika watakutana hapo kesho katika ngome kuu ya zamani ya waasi nchini Ivory Coast kwa sherehe ya kuadhimisha hatua muhimu kuelekea amani ya kudumu katika nchi hiyo iliogawika ya Afrika magharibi.

Rais Laurent Gbagbo atasimamia sherehe hizo za kusalimisha silaha kwenye makao makuu ya waasi ambazo pia zitahudhuriwa na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso,John Kufour wa Ghana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.

Viongozi wengine watakaohudhuria sherehe hizo pamoja na Waziri Mkuu wa Ivory Coast kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro ni Abdoulaye Wade wa Senegal,Faure Yassingbe wa Togo,Amadou Toumani Toure wa Mali na Yayi Boni wa Benin.

Gbagbo ambaye atakuwa anafanya ziara yake ya kwanza huko Bouake makao makuu ya kundi la waasi la zamani la FN tokea mwezi wa Septemba mwaka 2002 wakati uasi uliotaka kumpinduwa lipoigawa nchi hiyo pande mbili ametangaza siku ya kesho Jumatatu kuwa ni siku ya mapumziko ili kuwawezesha maelfu ya watu kuhudhuria sherehe hizo.