1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil mabingwa wa Marekani kusini

8 Julai 2019

Brazil wameunyakua ubingwa wa Amerika Kusini baada ya kuwalaza Peru 3-1 kwenye fainali ya Copa America iliyopigwa usiku wa Jumapili katika uwanja wa Maracana huko Brazil.

https://p.dw.com/p/3Ll01
Brasilien Copa America - Brasilien vs. Peru
Picha: Reuters/S, Moraes

Wenyeji Selecao waliingia uongozini katika dakika ya kumi na tano baada ya chipukizi Everton kuupachika wavuni mpira kufuatia krosi safi ya mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus.

Jesus alifunga bao la pili baada ya kuandaliwa na Everton kisha mshambuliaji wa klabu ya England Everton, Richarlison aliyeingia kama mchezaji wa akiba akafunga mkwaju wa penalti na kufanya mabao kuwa matatu.

Peru walifungiwa bao la kufutia jasho na Paolo Guerrero kupitia penalti baada ya Thiago Silva kuunawa mpira.

Kocha wa Brazil alimshambulia Lionel Messi

Hili lilikuwa taji la kwanza la Brazil tangu waishinde Copa America mwaka 2007 na pia taji la kwanza kabisa kwa kocha wao Tite.

Baada ya mechi hiyo Tite alimshambulia nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi yao na Chile Jumamosi alisema kwamba kuna njama zilizopangwa kuhakikisha kwamba Brazil wanashinda Copa America.

Fußball Brasilianischer Nationaltrainer Tite nach Gewinn der Copa America
Kocha wa Brazil Tite, alimshambulia Lionel MessiPicha: picture-alliance/Xinhua/X. Yuewei

"Mtu ambaye namfahamu kama mchezaji wa kipekee, Lionel Messi, anastahili kuwa na adabu kidogo. Na anastahili kuelewa na kukubali anapofungwa. Kwasababu katika mechi kadhaa tulishindwa na hata katika Kombe la Dunia. Kwa hiyo anastahili kuwa makini sana na anachosema. Ninatoa jawabu la moja kwa moja kwa yale aliyoyasema," alisema Tite.

Kocha wa Chile Ricardo Gareca kwa upande wake alikiri kushindwa.

"Ukweli ni kwamba Brazil walicheza vyema kutuliko. Ukweli ni kwamba ni timu bora kutuliko. Tulijaribu, tukafikia kiwango chao wakati mmoja. Tungetumia nafasi zetu vyema wakati mchezaji wao mmoja alipoonyeshwa kadi nyekundu lakini hatukuweza kwa kuwa kocha wao Tite alirekebisha kila kitu vyema na wakashinda," Gareca alisema.