1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZIL NA TANZANIA DAR-ES-SALAAM LEO

7 Juni 2010

Ujerumani yawasili Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/Nk7D
Nembo Kombe la Dunia 2010

Leo "asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu, atie gongo-mkutano Uwanja wa Taifa mjini Dar-esalaam":mabingwa mara 5 wa dunia, Brazil wamewasili kwa mpambano wao na Taifa Stars jioni hii.Ujerumani, imewasili nayo Afrika Kusini , baada ya kukataa kuruka na ndege yao Frankfurt bila mwanamuziki maarufu Shakira.

Afrika Kusini, ikitangaza itayari kwa changamoto za Kombe la Dunia,si chini ya mashabiki 15 wamejeruhiwa jana baada ya kuzika vurumai uwanjuani wakati wa mpambano wa kirafiki kati ya Nigeria na Korea ya Kaskazini.

Afrika kusini, ilitangaza jana kwamba, itayri kuandaa Kombe la kwanza la dunia barani Afrika huku rais wake Jacob Zuma, akisema mashindano haya yameonesha jinsi Taifa hili la makabila na rangi mbali mbali-(Rainbow Nation)-mwishoe,lilivyounagana pamoja.

Siku 5 kabla Bafana Bafana, haikupambana na Mexico, kufungua dimba la kombe la dunia 2010, Rais wa FIFA-Shirikisho la dimba ulimwenguni, Sepp Blatter,alinadi kwamba, Afrika kwa jumla, yafaa kuvuliwa kofia na kupewa heko kwa maandalio iliofanya na bara masikini kabisa halitaweza tena kutengwa upande.

Na wakati juhudi za kuwaunganisha waafrika kusini wa rangi na makabila mbali mbali katika kile Askofu Desmond Tutu alikiita "Rainbow Nation"- Taifa la makabila na rangi mbali mbali zilikumbwa na misukosuko kadhaa,rais Zuma kwamba, Mashindano ya Kombe la dunia nchini yamefanyaa maajabu kuwaunganisha watu wa makabila mbali mbali. Bendera za Afrika Kusini, ndizo zinazouza na kupepea mno madukani na mitaani.Rais Zuma akanadi kwamba, "Bafana Bafana " nayo iko tayari na imejiwinda kwa vita vya dimba."

TANZANIA DHIDI YA BRAZIL:

Jazba na homa ya kombe la dunia ikilikumba Taifa zima la Afrika Kusini na bila shaka Afrika nzima,si chini ya mashabiki 16 walijeruhiwa jana pale walipojaribu kusonga mbele kwa nguvu kuingia uwanjani mjini Johannesberg kuangalia mpambano wa kirafiki baina ya Super Eagles-Nigeria na Korea ya Kaskazini.Vurumai ikazuka ikisababishwa zaidi na mashabiki wa Nigeria, waliotaka kumiminika kwea nguvu katika uwanja unaochukua mashabiki 10.000 tu.

Mkasa huu wa kusikitisha ,ulitokea katika siku ambayo timu nyingi za taifa pamoja na Ureno ikiongozwa na Cristano Ronaldo, zikiwasili.

Baada ya kuchelewa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Frankdfurt jana usiku kutokana na kuchelewa kwa abiria mashuhuri,mwimbaji mashuhuri Shakira,atakae watumbuiza mashabiki huko Soweto alhamisi hii ,kikosi cha Ujerumani, kikiongozwa na kocha wao Joachim Löw kilitua Johannesberg na ndege mpya kabisa na ya kifahari ya LUFTHANSA:

Akitangaza kwamba, wachezaji wake wote aliowasili nao ni fit kwa changamoto za Kombe la dunia,Löw,alisema kwamba, kila mmoja anatarajia sasa kujionea mambo yatakuaje na kujionea binafsi mandhari ya nchi hii ya Afrika Kusini. Ujerumani , inapiga kambi yake mjini Pretoria.

Kabla ya kuwasili,kocha Joachim Löw ,alisema,

"Kuanzia jumatatu tutakuwa tayari nchini Afrika Kusini na hapo hapo tutaanza mazowezi yetu ya kawaida na kujirekebisha na hali ya hewa ya nyanda za juu."

Kuhusu matumaini ya Ujerumani, iliowasili na timu ya chipukizi ikiongozwa na nahodha Philipp Lahm, alisema,

"Tuna matumaini makubwa.Daima tunapokwenda katika Kombe la Dunia huwa na matumaini makubwa ya ushindi."

Ujeruimani, imeangukia kundi D na itafungua dimba Jumapili hii ijayo na Australia, mjini Durban,kabla kucheza na Serbia na mwishoe, Black Stars-Ghana.

Mabingwa mara 5 wa dunia-Brazil walikwisha wasili Afrika Kusini, kuania taji la 6.Jana usiku, Brazil iliwasili Dar-es-salaam,Tanzania ambako kila mmoja ameingiwa na homa ya Kombe la dunia kana kwamba, linaaniwa Tanzania.Mashabiki waliolalalamika hapo awali kuwa Tiketi ni za bei za juu walisheheni katika vituo vya kununulia tiketi.Ili kuiwasaidia mashabiki , baadhi ya makampuni na klabu za dimba nchini, zimenunua tiketi ili kuwapa mashabiki wao na Uwanja wa Benjamin Mkapa unaochukua mashabiki 60.000 unatazamiwa kujaa pomoni jioni hii.

Upande wa pili wa mpaka nchini Kenya, Harambee Stars ,walitamba kwa mabao 2:1 mbele ya Ugandan Cranes katika duru ya tatu ya Kombe la Afrika.

Mwandishi: Ramadhan Ali/DPAE/AFPE

Uhariri:Josephat Charo