1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brexit kupigiwa kura ya tatu Uingereza

Sekione Kitojo
29 Machi 2019

Iwapo mfumo wa  kisiasa  nchini  Uingereza  utashindwa  kuvunja mkwamo wa Brexit  Ijumaa, nchi  hiyo itakabiliwa  na uwezekano  wa  kujitoa  katika  Umoja  wa  Ulaya  bila  makubaliano hapo  Aprili 12.

https://p.dw.com/p/3FrUt
UK Brexit | Parlament
Bunge la Uingereza katika kikao chakePicha: AFP/PRU/HO

Wabunge watapata  fursa  ya  tatu leo kuyapigia  kura makubaliano ya  kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya. 

Makubaliano  hayo  hata  hivyo yamekabiliwa  na  upinzani  mkubwa , hata  baada  ya  May  kuamua  kuiweka rehani  kazi  yake ili makubaliano  hayo  yapite, na  kuahidi  kujiuzulu  iwapo  wabunge wataidhinisha  makubaliano  hayo na  kuiacha Uingereza  ijitoe kutoka  Umoja  wa  Ulaya  kama  ilivyopangwa  mwezi  Mei.

England, London: Debatte im House of Commons
Waziri mkuu Theresa May akilihutubia bunge Machi 27, 2019Picha: Reuters/UK Parliament/M. Duffy

Mpambano  wa  vuta nikuvute  nchini  humo kuhusu Brexit umesababisha  bunge  la  nchi  hiyo  kugawanyika na  kuunda vikundi  hasimu  ambavyo  dhamira yake  na  ajenda  zinapitia  katika misingi  ya  asili  ya  chama  hicho.

Waziri  mkuu Theresa  May atajaribu  kuwa mchungaji  wa  makundi hayo  yanayovutana na  hatimaye kupata  wingi  ambao kila  mara unakosekana ambao utaweza  kufanikisha  makubaliano  yake  ya talaka  na  Umoja  wa  Ulaya  katika  jaribio  la  tatu  leo  Ijumaa , siku ambayo  nchi  hiyo  ilitamka  kwamba  itajitoa  rasmi  katika Umoja  huo, siku  ya  Brexit.

Großbritannien London Andrea Leadsom bei Erklärung zum Rückzug
Andrea Leadsom kiongozi wa wabunge wa chama cha Conservative bungeniPicha: Getty Images/C. Court

Kiongozi wa baraza  la  wawakilishi  la  Uingereza  Andrea Leadsom akitangaza  kuhusu  kura  hiyo  jana  alisema.

"Kama  nilivyoliambia  bunge  wakati  nikitoa  taarifa  yangu mapema leo, hoja iliyowasilishwa na  serikali mchana  huu imetayarishwa  ili kuweza  kufuatana  na uamuzi  wako, Bwana  Spika, wakati  huo  huo ukiakisi  nia  ya  Umoja  wa  Ulaya kukubali tu  kurefusha  kifungu 50 hadi  tarhe  22  mwezi Mei iwapo  makubaliano  ya  kujitoa yataidhinishwa  ifikapo mchana Machi 29."

Tatizo  la  May

Tatitzo  la  May  linatokana  na  kushindwa  kwake  kudhibiti wabunge wa  chama  chake  cha  Conservative. Chama  hicho  ambacho kimsingi  kinapendelea  wafanyabiashara hakikubaliani  kuhusu iwapo  Brexit  ni  mzuri kwa  Uingereza, mtazamo  ambao  May binafsi si mara  zote  amekubaliana  nao, na  iwapo  Brexit inapaswa  kulegezwa  ama  kuendewa  kama  ilivyo.

Theresa May
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: Getty Images/J. Taylor

Wapinzani  wa  dhati  ya  Umoja  wa  Ulaya  walijaribu  kumuondoa madarakani  May mwezi  Desemba  na kisha  wakasaidia  kushindwa kwa  makubaliano  aliyofikia  katika  kura  iliyopigwa  mwezi  Januari na  kupata  kipigo  cha  kihistoria  kwa  kura  432 dhidi  ya  202.

Zaidi  ya  theluthi  ya  wabunge  wa  chama  hicho  wapatao 313 walipiga  kura  kupinga  makubaliano  aliyofikia  May  na  Umoja  wa Ulaya  kila  mara yalipofikishwa  bungeni.

Birmingham Boris Johnson Rede auf Parteitag Konservative Partei
Boris Johnson anawania kiti cha mwenyekiti wa chama cha ConservativePicha: Getty Images/J.J. Mitchell

Idadi ya waasi  ilipungua  kwa  robo wakati mpango  wake uliposhindwa  tena kwa  kura 391 dhidi  ya  242  hapo Machi 12. Kiongozi anayeonekana kuwania  kiti cha  May  katika  chama  Boris Johnson  amesema ahadi  ya  May  siku  ya  Jumatano ya  kujiuzulu iwapo makubaliano  yake  yataidhinishwa ina  maana  kwamba, "itabidi  niunge  mkono kitu  hicho".