1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRISBANE:Mwengine akamatwa kuhusika na mashambulizi ya Uingereza

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmE

Mtu mmoja amekamatwa huko Australia akishukiwa kuhusika na jaribio la shambulizi la kigaidi katika miji ya London na Glasgow huko Uingereza,na kufanya idadi ya washukiwa waliyokamatwa mpaka sasa kufikia wanane.

Maafisa wa Australia wamesema kuwa mshukiwa huyo alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Brisbane hapo jana akitaka kusafiri.

Wakati huo huo washukiwa wawili waliyokamatwa huko Uingereza wamebainika kuwa ni madaktari kutoka Iraq na Jordan, na maafisa wanaamini kuwa huenda washukiwa wengine pia wakawa ni raia wa nje.

Kiwango cha hali ya tahadhari nchini Uingereza ni cha juu.

Nchini Ufaransa polisi wamewakamata washukiwa watatu wanachama wa kundi haramu la Basque wakijiandaa kuingia Uhispania wakiwa na gari lililojaa milipuko.

Watu hao walikamatwa katika mji wa bandari wa Saint Jean Pied wakiwa na zaidi ya kilogramm 160 za madawa yakulipuka, mitungi miwili ya gas pamoja na silaha.