1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mataifa ya Ulaya yafurahishwa na uamuzi wa Wolfowitz wa kujiuzulu.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0t

Mataifa ya Ulaya magharibi yameeleza kufurahishwa kwao kuhusiana na uamuzi wa rais wa benki ya dunia Paul Wolfowitz kujiuzulu na kazi ya kumsaka mridhi wake imeanza rasmi.

Marekani , ambayo inateua rais wa benki hiyo, imesema itachukua hatua haraka kumpaka rais mpya badala ya Wolfowitz.

Ametangaza siku ya Alhamis kuwa atajiuzulu mwishoni mwa mwezi wa Juni kutokana na kashfa inayomkabili kwa kupanga kumpandisha cheo na mshahara mnono mpenzi wake wa kike, ambaye ni mwajiriwa wa benki hiyo.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrück amesema kuwa naibu waziri huyo wa zamani wa ulinzi wa Marekani amechukua uamuzi sahihi katika kujiuzulu wakati kashfa hiyo imeathiri heba ya taasisi hiyo ya benki ya dunia.