1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mataifa ya Ulaya yashutumu makubaliano.

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGk

Nchi kadha za Ulaya zimeyakosoa makubaliano yanayodaiwa , kati ya serikali ya Afghanistan na viongozi wa Taliban ambayo yamesababisha kuachiwa huru kwa mwandishi habari wa Kitaliani siku ya Jumanne.

Daniele Mastrogiacomo alishikiliwa na Taliban kwa muda wa wiki mbili.

Wateka nyara wake wamesema wamemwachia baada ya serikali ya Afghanistan kuwaachia viongozi kadha wa Taliban kutoka jela. Mataifa ya magharibi , ikiwa ni pamoja na Ujerumani na Uholanzi , yameonya kuwa hatua hiyo ni ya hatari.