1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mwito kwa Umoja wa Ulaya kusaidia zaidi Afghanistan

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt0

Uingereza na Uholanzi zimewahimiza washirika wao katika Umoja wa Ulaya wasaidie zaidi kuleta hali ya utulivu nchini Afghanistan.Lakini Ufaransa inachukua hatua ya tahadhari kuhusu mwito wa NATO kwamba ujumbe wa Umoja wa Ulaya usaidie kujenga sekta ya polisi na sheria nchini Afghanistan. Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesema ujumbe utapelekwa Afghanistan kuchunguza vipi operesheni ya kutoa mafunzo itaweza kusaidia.Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesema anakaribisha msaada zaidi wa Umoja wa Ulaya kwa maafisa wa polisi 40 wa Kijerumani ambao hivi sasa nchini Afghanistan wanatoa mafunzo kwa vikosi vya nchi hiyo.Katibu mkuu wa NATO,Jaap de Hoop Scheffer takriban kila siku alikuwa akitoa mito kwa Umoja wa Ulaya kusaidia zaidi kubeba mzigo nchini Afghanistan.