1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. NATO haingi kuwekwa ngao dhidi ya makombora.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8p

Washirika wa NATO wametoa uungaji wao mkono kwa mipango yenye utata ya Marekani ya kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora katika Ulaya ya mashariki.

Katika mkutano mjini Brussels, mataifa wanachama wa pia wamekubaliana kuwa mfumo wowote wa hapo baadaye wa ngao dhidi ya makombora unapaswa kusaidia mfumo huo wa Marekani ili kuhakikisha kuwa Ulaya nzima inakingwa.

Katibu mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer amesema kuwa mataifa ya NATO hayana kipingamizi.

Hata hivyo , serikali ya Russia inaendelea kupinga wazo hilo la kuwa na mkakati wa mfumo wa ulinzi wa Marekani karibu na mipaka yake.

Marekani inasisitiza kuwa uwekaji wa mfumo huo nchini Poland na jamhuri ya Chek si tishio kwa Russia na unaweza kutumika kulinda sehemu za Ulaya dhidi ya makombora yatakayorushwa kutoka mashariki ya kati.