1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Nchi masikini kuathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC1

Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani imesema kwamba nchi masikini ndio zitakazo athirika zaidi na mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

Jopo la serikali mbali mbali linaloshuhgulikia mabadiliko ya hali ya hewa lilikesha usiku kucha kabla ya kukubaliana juu ya maneno yatakayotumiwa katika ripoti yake huko mjini Brussels, Ubelgiji.

Ripoti hiyo imelaumu gesi chafu zinazosababishwa na binadamu kuwa zimefikia kiwango cha juu.

Ripoti hiyo imesema kuwa kuenea kwa jangwa, ukame na kuongezeka kina cha maji ya bahari kutaathiri zaidi nchi za joto na nchi za Afrika zilizo katika maeneo ya jangwa mpaka katika visiwa vya Pacific.

Jopo hilo la umoja wa mataifa linaloshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa linawajumuisha wanasayansi 2,500 kutoka nchi zaidi ya 100.