1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Putin asitisha majumu ya mkataba.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6X

Rais wa Russia Vladimir Putin ametangaza jana kuwa nchi yake inasitisha majukumu yake chini ya mkataba wa kudhibiti silaha za kawaida uliotiwa saini kati ya nchi hiyo na mataifa ya Ulaya.

Katibu mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer ameeleza wasi wasi wake mkubwa kwa uamuzi huo wa rais Putin.

Makubaliano hayo yalikuwa na lengo la kufikia upunguzaji mkubwa wa vifaa vya kijeshi katika bara la Ulaya.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema ni muhimu kwa Ulaya kuzuwia kutumbukia zaidi katika hali ya shaka shaka kati ya Marekani na Russia. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amerudia kuwa mpango wa mradi wa ulinzi dhidi ya makombora utakaowekwa katika mataifa ya Ulaya mashariki hauilengi Russia.

Mataifa ya NATO hayajaidhinisha makubaliano ya kudhibiti silaha , CFE, yakisisitiza kuwa Russia kwanza iondoe majeshi yake yaliyobaki kutoka Georgia na Moldova.