1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Steinmeir akanusha suala la Kurnaz

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYQ

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amekanusha kwamba hapo mwaka 2002 serikali ya Kansela wa Ujerumani wa zamani Gerhard Schröder ilipuuza pendekezo la Marekani la kumuachilia huru Mturuki mzalia wa Ujerumani aliekuwa akishikiliwa huko Guantanamo nchini Cuba.

Hayo yamethibitishwa na kamati maalum ya bunge la Umoja wa Ulaya ambayo repoti yake ya mwisho inahitimisha kwamba mahabusu huyo wa zamani kwenye gereza la Guantanamo Murat Kurnaz sio tishio la ugaidi.Steinmeir ambaye wakati huo alikuwa waziri wa nchi katika ofisi ya Kansela amesema mjini Brussels kwamba kuwasiliana kwa Ujerumani na Marekani na Uturuki kutaka kuachiliwa kwa Kurnaz kulingia tu hatua muhimu hapo mwaka 2005.

Kurnaz ambaye alikamatwa nchini Pakistan hapo mwaka 2001 akiwa mtuhumiwa wa ugaidi na kupelekwa Guantanamo Cuba hatimae aliachiliwa huru mwezi wa Augsuti mwaka jana.

Hakuwahi kufunguliwa mashtaka.