1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya yafuatilia safari za siri za CIA

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYN
Soko la hisa mjini Frankfurt
Soko la hisa mjini FrankfurtPicha: AP

Kamati ya bunge ya Umoja wa Ulaya imesisitiza madai yake kwamba hadi mataifa 13 ya Umoja wa Ulaya yalikuwa yakijuwa juu ya safari za siri za Marekani barani Ulaya na kukamatwa kwa watuhumiwa wa ugaidi na mashushu wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA.

Ikirekebisha repoti yake ya awali ya mwezi wa Novemba kamati hiyo imesema hivi sasa hakuna ushahidi wa kutosha kwamba kuna magereza ya siri ya CIA nchini Poland.Kamati hiyo imesema imegunduwa kuwepo kwa safari za siri 1,400 hususan kupitia Uingereza,Ujerumani na Ireland nyingi ya safari hizo zikiwa ni kwa ajili ya kile kinachoitwa kuwa dhamira ya kurudisha wafungwa kutoka nchi moja kwenda nyengine.

Kiongozi wa kamati hiyo Carlos Coelho pia ameushutumu uongozi wa juu wa Umoja wa Ulaya kwa kukataa kutowa nyaraka za bunge la umoja huo kuhusu mawasiliano kati ya Umoja wa Ulaya na maafisa wa CIA.

Kamati hiyo ilianza uchunguzi wake hapo mwaka 2005 juu ya madai kwamba CIA ilikuwa ikiwashikilia watuhumiwa wa kundi la Al Qaeda barani Ulaya bila ya kuzingatia mchakato wa sheria.

Makubaliano ya haki za binaadamu ya Umoja wa Ulaya yanahakikisha kuwepo kwa mashtaka yanayozingati haki.