1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya huenda ukaruhusi wahamiaji halali kutoka Afrika.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaE
Vigogo wawili wapinzani wa Marekani marais Hugo Chavez na Mahmoud AhmedNejad
Vigogo wawili wapinzani wa Marekani marais Hugo Chavez na Mahmoud AhmedNejadPicha: AP

Katika mkutano usiokuwa rasmi wa mawaziri wa mambo ya ndani na wa sheria wa umoja wa Ulaya , kundi hilo la mataifa limeonyesha ishara kuwa litafungua njia kwa wahamiaji halali kwa mara ya kwanza.

Lakini waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameongeza kuwa mtazamo utakuwa kuwapa wageni nafasi za uhamiaji wa muda tu kusaidia kupambana na upungufu wa wafanyakazi katika bara la Ulaya.

Kamishna wa umoja wa Ulaya anayehusika na sheria Franco Frattini amesema kuwa mataifa ya Afrika yatachaguliwa katika muda wa wiki chache zijazo kwa ajili ya kujadili mipango ya mwanzo juu ya wahamiaji halali.

Frattini pia ameyataka mataifa wanachama kuongeza ushirikiano ili kuweza kulinda mipaka ya eneo la bahari ya Mediterranean, na kuonya kuwa umoja wa Ulaya utakabiliwa hivi karibuni na wahamiaji haramu wengi watakaowasili katika nchi hizo.