1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya kutekelza vikwazo dhidi ya Iran

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYf

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wameamua kutekeleza kikamilifu vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. Hii inafuatia hatua ya Iran kukataa kukomesha urutubishaji wa madini yake ya uranium.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha vikwazo hivyo mnamo tarehe 23 mwezi Disemba mwaka jana na likaipa Iran siku 60 kutii. Tangazo la Umoja wa Ulaya limetolewa huku Iran ikisema wachunguzi 38 wanaoufanyia kazi Umoja wa Mataifa wamekatazwa wasiingie Iran. I

ran inashikilia kwamba mpango wake wa nyuklia ni wa kutengeza nishati ya umeme, lakini Marekani na Umoja wa Ulaya zinahofu huenda Iran inajaribu kutengeza bomu la nyuklia.

Wakati huo huo mawaziri wa Umoja wa Ulaya wameitaka serikali ya Sudan iruhusu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waingie katika eneo la Darfur kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani kwenye eneo hilo.

Hata hivyo mawaziri hao hawakukubaliana juu ya msaada wa kifedha kulisaidia jeshi la Umoja wa Afrika lililo Darfur.