1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya waandaa kikao kuhusu Somalia

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdc

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, anaongoza mkutano wa mataifa ya Ulaya wanachama wa kundi la mataifa yanayoshughulikia mzozo wa Somalia.

Mataifa hayo ni Uingereza, Italia, Sweden na Norway.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Javier Solana pamoja na Msimamizi wa umoja huo wa maendeleo na misaada ya kiutu, Louis Michel, wamealikwa kuhudhuria kikao hicho.

Taarifa iliyotolewa na Ujerumani imesema lengo la kikao hicho ambacho si rasmi ni kutathmini hali ilivyo sasa nchini Somalia na pia kuratibu juhudi za Umoja huo nchini humo.