1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya waishinikiza Sudan ikubali kikosi cha kijeshi cha Umoja wa mataifa

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1l

Umoja wa Ulaya umeishinikiza serikali ya Sudan kusimamisha machafuko yanaoendelea kulikumba eneo la Darfur magharibi mwa nchi, kwa kukubali kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa mataifa cha kulinda amani kipelekwe katika jimbo hilo.

Hadi sasa Sudan inapinga kutumwa kwa kikosi cha wanajeshi 20,000 wa kimataifa kushika nafasi ya kikosi cha wanajeshi 7,000 kutoka Afrika ambao hawana vifaa vya kutosha. Mnamo miaka mitatu iliopita ya mzozo, inakisiwa kuwa watu 200,000 waliuawa na wengine milioni 2,4 waliyahama maskani yao.