1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya watakiwa kutofanya pupa katika upanuzi wa umoja huo.

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjF

Rais wa tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso ameuonya umoja wa Ulaya kutofanya haraka kupanua umoja huo. Akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa umoja wa Ulaya mjini Brussels, Barroso amesema ni muhimu kuwa umoja wa Ulaya unabaki na uwezo wake wa kufanyakazi kwa ufanisi. Viongozi wa umoja wa Ulaya pia wameidhinisha uamuzi wa kusitisha kwa muda mazungumzo ya uanachama wa Uturuki katika umoja huo kutokana na nchi hiyo kukataa kufungua bandari na viwanja vyake vya ndege kwa vyombo vya usafiri vya Cyprus ambayo ni mwanachama wa umoja wa Ulaya.

Hapo mapema mjini Berlin , kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametumia hotuba yake bungeni kuainisha nia ya nchi yake wakati wa miezi sita ya urais katika umoja wa Ulaya unaoanza Januari mosi. Merkel amesema lengo kuu litakuwa kupata katiba ya umoja wa Ulaya na kuliangalia suala la nishati na masuala ya mazingira.