1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wazindua mapendekezo ya sera ya nishati.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbj

Umoja wa Ulaya umezindua mapendekezo ambayo endapo yataidhinishwa yatausaidia Umoja huo kuandaa sera ya pamoja ya Ulaya ya nishati.
Mapendekezo hayo yanajumuisha kuongeza njia za kupata nishati na pia kupunguza gesi za viwandani kwa asilimia 20 kufikia mwaka 2020.

Rais wa tume ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba taratibu hizo zitausaidia Umoja wa Ulaya kuongoza katika harakati za kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Mapendekezo hayo yametangazwa siku chache baada ya Russia kukatiza mafuta yake yanayosambazwa katika mataifa kadha ya Ulaya, hatua ambayo imezua tena hali ya wasiwasi kuhusu uwezo wa mataifa ya Ulaya kujimudu kwa nishati.