1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Viongozi wa Ulaya wakubali sera ya nishati

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKz

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kimsingi kuunga mkono sera ya matumizi ya nishati yenye lengo la kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa dunikani.

Kansela Angela wa Merkel wa Ujerumani ambaye nchi yake inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya amesema hayo hapo jana pamoja na kutahadharisha kwamba jinsi ya kufanikisha malengo ya mpango huo itabidi kujadiliwe zaidi.Amesema viongozi wa Umoja wa Ulaya watajadili mahsusi namna ya kushirikiana mzigo huo wa kufanikisha malengo ya kujifunga juu ya nishati zinazoweza kutumika upya wakati watakapokutana leo hii katika siku ya pili ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Mapema Merkel alitaka Umoja wa Ulaya uongoze njia katika vita dhidi ya kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Wito wake wa kuwepo kwa malengo ya kijifunga ambayo yanataka nishati zinazoweza kutumiwa upya kama vile nguvu za upepo na jua au kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ziwe asilimia 20 ya matumizi ya nishati ifikapo mwaka 2020 umekabiliwa na upinzani mkali kutoka nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya pia wanatarajiwa kuidhinisha lengo la kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira duniani kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2020.