1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Virusi vya H5N1 vyathibitishwa Uingereza

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVO

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imesema,uchunguzi wa maabara umethibitisha kuwa virusi vya H5N1 vya homa ya mafua ya ndege vimekutikana mashariki mwa Uingereza,katika shamba linalofuga bata mzinga. Shamba hilo lenye mabata mzinga 160,000 ni shamba kubwa kabisa la aina hiyo barani Ulaya na kuna uwezekano kuwa mabata wote watauliwa.Madaktari wa mifugo waliitwa kwenye shamba hilo siku ya Alkhamisi,baada ya mabata mzinga 2,500 kufariki.Hii ni kesi ya pili ya virusi vya H5N1 kuthibitishwa mwaka huu katika Umoja wa Ulaya. Hivi karibuni,virusi hivyo vilikutikana nchini Hungary.Wataalamu wana hofu kuwa virusi vinavyosababisha homa ya mafua ya ndege huenda vikabadilika na kuambukiza binadamu.Tangu mwaka 2003,homa ya mafua ya ndege kote duniani,imeua watu 164.Idadi kubwa ya vifo hivyo vilitokea katika nchi za Asia.