1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:ICG yapendekeza majeshi yasalie Kongo

10 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCc1
Shimon Peres anamatumaini ya kuchaguliwa rais mpya
Shimon Peres anamatumaini ya kuchaguliwa rais mpyaPicha: AP

Ripoti ya Shirika lisilo la kiserikali la International Crisis Group,ICG inasisitiza kuwa majeshi alfu 17 ya Umoja wa Mataifa yanahitajika kuendelea kubakia nchini Kongo mpaka mwisho wa mwaka huu ili kudumisha usalama na ustawi.

Shirika hilo lililo na makao yake Brussels,Ubelgiji linasema kuwa amani na usalama utadumishwa nchini Kongo endapo jamii ya kimataifa itaendelea kutoa rasilmali na ufadhili kwa nchi hiyo.Aidha inatoa wito kwa wafadhili wa kimataifa kuunda mpango mpya wa misaada ili kusaidia wakazi wa nchi hiyo kurejea katika maisha ya sawasawa kufuatia kipindi kirefu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe.Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ilifanya uchaguzi wa kidemokrasia wa kihistoria mwaka jana baada ya kipindi cha miaka 40.Uchaguzi huo ulimpa ushindi Rais Joseph Kabila wa chama cha PPRD.