1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels.Ischinger ateuliwa kushiriki mazungunzo juu ya Kosovo.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdv

Umoja wa Ulaya umemteua mwanadiplomasia wa Ujerumani Wolfgang Ischinger kuwakilisha kundi hilo la mataifa 27 katika majadiliano yajayo juu ya hali ya baadaye ya jimbo la Serbia la Kosovo.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana amesema katika taarifa kuwa Ischinger atajiunga na wawakilishi kutoka Marekani na Russia, ambao watakuwa wapatanishi katika mazungumzo hayo.

Serbia inakataa mpango wa umoja wa mataifa ambao unatoa uhuru kwa jimbo la Kosovo chini ya uangalizi wa kimataifa.