1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS.Mawaziri wa biashara wa nchi za umoja wa ulaya wakutana

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQi

Kamishna wa viwanda wa umoja wa ulaya Günter Verheugen anakutana na mawaziri wa biashara wa umoja wa ulaya mjini Brussels kujadili juu ya uwezekano wa kupunguza urasimu katika nchi wanachama wa umoja wa ulaya.

Bwana Verheugen anataka nchi hizo 27 wanachama wa umoja wa ulaya zipunguze sheria ili kuwezesha kiwango cha Euro bilioni 150 katika uwekezaji.

Baadhi ya nchi wanachama zina wasiwasi kwamba hatua hiyo itasababisha kuzorota kwa hali ya usalama na kijamii. Waziri wa biashara wa Ujerumani Michael Glos amesema kuwa Uholanzi ichukuliwe kama mfano wa upunguzaji wa rasimu.