1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Merkel ataka usawa wa kijnsia barani Ulaya

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL8

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa mwanamke wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 iliyopita, kuongoza mkutano wa kilele wa wakuu wa Umoja wa Ulaya, ametaka kuwepo kwa usawa wa kijinsia barani Ulaya.

Kansela Merkel amesema kuwa usawa wa jinsia iwe ni suala muhimu katika juhudi za Ulaya kuwa kileleni kiuchumi duniani katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Katika siku hii ya wanawake duniani, Umoja wa Ulaya umeahidi, kupambana na ukandamizwaji na unyanyasaji majumbani dhidi ya wanawake.

Mapema Kansela Merkel alifungua maonesho ya picha 65 za wanawake mashuhuri, na kusema kuwa Ulaya haiwezi kuwa imara bila ya nafasi ya wanawake katika jamii.

Kwa upande mwengine Kansela huyo wa Ujerumani alisema Ulaya ni lazima iwe msari wa mbele katika mapambano dhidi ya uchafuzi wa hali ya hewa.