1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga yarudi uwanjani leo

30 Januari 2009

Hoffenheim inaongoza ikiwa na miadi na Cottbus.

https://p.dw.com/p/GkAQ
Bayern munich(Nyeusi) mabingwa.Picha: picture-alliance / dpa

Kesho ama Kamerun au Ghana itaibuka mabingwa wa Kombe la Afrika la chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mjini Kigali-

Viongozi wa Ligi pale msimu wa Bundesliga ulipoenda likizo ya X-masi na mwaka mpya, Hoffenheim wana miadi leo na Energie Cottbus bila ya stadi wao Ibisebic alietia mabao 18.

Katika premier League,Manchester United inaongoza Ligi kwa pointi 2 na FC Barcelona inataka kuvunja rekodi ya magoli iliowekwa na real Madrid msimu wa 1989/90.

Kesho ni finali ya kombe la vijana la Afrika kati ya simba wa nyika-Kamerun na chipukizi wa Black Stars-Ghana mjini Kigali,Ruanda.

Finali hii inatanguliwa na changamoto jioni hii ya kuania nafasi ya 3 baina ya mabingwa mara 5 Nigeria na Afrika Kusini,timu 2 zilizokwisha kutana duru za awali.

Firimbi ililia jana usiku kuanzisgha mjini Hamburg duru ya pili ya msimu wa Bundesliga kati ya mabingwa Bayern Munich na Hamburg iliopo nafasi ya tatu au changamoto kati ya wababe wa kusini na wa kaskazini.

Mla, lakini, ni mla leo, mla jana anasema Oumilkheir kala nini:

Viongozi wa Bundesliga-klabu chipukizi ya Hoffenheim iliopanda msimu huu daraja ya kwanza inatazamiwa leo kuendeleza maajabu yake ikiwa bado kileleni mwa Bundesliga.Ikicheza nyumbani na Cottbus, Hoffenheim,iko uwanjani leo bila ya mshambulizi wake hatari Vedad Ibisevic kutoka Bosnia, aliepachika jumla ya mabao 18 kutoka mechi 17.Ibisevic ameumia.kujaza pengo lake,Hoffenheim imemuazima kutoka Bremen,mshambulizi wa Kamerun Boubacar Sanogo.

Kocha Ralf Rangnick hawezi pia kumteremsha stadi wao mwengine, mbrazil Carlos eduardo aliefungiwa mechi 2 baada ya kutolewa nje ya uwanja kwa kupigana na Ivica Olic wa Hamburg.

Hertha Berlin, iliomaliza duru ya msimu huu iliopita ikiwa nafasi ya 3 ina miadi na Frankfurt.Changamoto nyengine leo ni kati ya FC Cologne na Wolfsburg na majirani zao Bayer Leverkusen wanacheza na Borussia Dortmund.

Kesho jumapili,Hanover inaikaribisha nyumbani schalke wakati Stuttgart waliozabwa majuzi mabao 5-1 na mabingwa Bayern Munich katika kombe la shirikisho la dimba, wanaonana na Borussia Moebnchengladbach. Bremen ilioanza msimu huu kwa kupepesuka wana miadi kesho na majirani zao Armenia Bielefeld.

Katioka Premier League-ligi ya uingereza, mabingwa manchester united wanaongoza Ligi kwa pointi 2 wakati Chelsea na Liverpool zinazokutana kesho zikifuata nyuma.Aston villa iko pointi 1 tu nyuma yao.

Huko Spian,FC barcelona inaendelea kuongoza Ligi kwa pointi 9 na inaelekea kuivunja rekodi ya Real Madrid ya mabao 107 iliotia msimu wa 1989/90.

Huko Itali,Inter Milan bado iko kileleni.

Kesho ni finali ya wanaume ya Australian Open,ubingwa waTennis wa Australia. Baada ya finali ya mapema hii leo ya wasichana kati ya Muamerika. Serena williams, na Mrus,i Dinara Safina,macho sasa yanakodolewa finali ya wanaume hapo kesho kati ya bingwa wa mabingwa Mswisi, Roger Federer, na Mspain, Rafael Nader au Fernando Verdasco.

Kuwasili finali ya kesho,stadi huyo wa Uswisi aliendelea na tabia yake ya kumbomoa Andy Rossick na kukata tiketi yake ya 18 ya finali ya Grand Slam.alimtimua kwa seti tatu-6-2,7-5 na 7-5. Akishinda kesho, Roger Federer atasawazisha rekodi ya Grand slam 14 alioiweka Pete Sampras wa Marekani.

Federer ameshiriki katika finali 13 kati ya 14 zilizopita za Grand Slam pamoja na kuweka rekodi ya kushinda grand slam 10 mfululizo-rekodi ambayo ilikomeshwa mwaka jana huko huko Melbourn,Ausrtralia pale Novak Djokovic alipomuangusha.