1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge kupigia kura makubaliano ya kugawana madaraka

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJif

NAIROBI:

Bunge la Kenya linakutana hii leo kupigia kura makubaliano ya amani yenye azma ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliozuka nchini humo kufuatia uchaguzi wa rais Desemba mwaka jana.Bunge linapaswa kupitisha sheria,ili makubaliano ya kugawana madaraka yaweze kuingia kazini.

Makubaliano yaliyopatikana juma lililopita,yanatoa mwito kwa Rais Mwai KIbaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kugawana madaraka,baada ya pande zote mbili kudai kuwa zilishinda uchaguzi wa rais uliofanywa Desemba 27.Mzozo huo ulisababisha umwagji damu na zaidi ya watu 1,000 waliuawa na maelfu wengine wamepoteza makaazi yao.