1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la India kuidhinisha sheria mpya kuhusu Kashmir

Oumilkheir Hamidou
6 Agosti 2019

Bunge la India litaidhinisha mswaada wa sheria utakaobatilisha kanuni za sehemu ya jimbo la Kashmir inayosimamiwa na India katika milima ya Himalaya. Pakistan nayo inajiandaa kuitisha maandamano kupinga uamuzi wa India.

https://p.dw.com/p/3NPWA
Indien Kaschmir-Konflikt nach Änderung Artikel 370
Picha: AFP/R. Bakshi

Serikali ya wahindu wanaopigania uzalendo, inayoongozwa na waziri mkuu Narendra Modi imewasilisha mswaada wa sheria kuhusu muundo mpya wa jimbo la Jammu na Kashmir katika bunge la Lok Sahba, siku moja baada ya hatua zilizochukuliwa sambamba na amri iliyotiwa saini na rais ya kubatilisha kifungu maalum kinachodhamini utawala maalum wa ndani katika jimbo hilo.

Hali si bayana katika jimbo hilo baada ya serikali kuzifunga njia zote za mawasiliano na ulimwengu wa nje, ikiwa ni pamoja na internet, simu za mkononi na nyenginezo.Serikali iemtuma maelfu ya wanajeshi katika eneo hilo linalopakana na milima ya Himalaya kwa hofu ya kuzuka machafuko.

Bunge linatarajiwa kuidhinisha bila ya shida yoyote mswaada huo wa sheria unaobatilisha kanuni za jimbo la Kashmir na kuligeuza kuwa jimbo la kawaida, sawa na majimbo yote mengine ya India.

Baraza la Senet limeidhinisha mswaada huo kwa wingi wa thuluthi mbili baada ya wawakiilishi wengi wa upande wa upinzani kuwaunga mkono wawakilishi wa chama tawala cha Bharatiya Janata Party.

Wasi wasi umetanda katika eneo la mpakani linaloigawa Kashmir kati ya India na Pakistan, ambazo zote kila moja inadai Kashmir ni sehemu ya ardhi yake.

Vikosi vya usalama vinalinda mpaka unaoigawa Kashmir kati ya India na Pakistan
Vikosi vya usalama vinalinda mpaka unaoigawa Kashmir kati ya India na PakistanPicha: AFP/R. Bakshi

Maandamano yanaitishwa katika miji tofauti ya Pakistan

Rais Arif Alvi wa Pakistan ameitisha kikako cha bunge mjini Islamabad kuzungumzia uamuzi wa ghafla wa india kuhusu Kashmir baada ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Pakistan kuukosoa uamuzi huo na kuutaka Umoja wa mataifa utume uchunguzi katika jimbo hilo. Mabaraza yote mawili ya bunge la Pakistan yanatarajiwa kupiga kura kupinga uamuzi wa India.Wakati huo huo viongozi wa kijeshi wa Pakistan wanakutana mjini Rawalpindi kuzungumzia mabadiliko ya kanuni za Kashimir.Vikosi vyote vya jeshi la Pakistan vimewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia ripoti za kutumwa wanajeshi ziada wa India huko Kashmir. Maandamano pia yataitishwa  katika miji ya Muzaffarabad, Lahore, Karachi na katika mji mkuu islamabad .Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezisihi pande hizo mbili zijizuwie.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/Afp

Mhariri: Sekione Kitojo