1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Senate kupigia tena kura mswada wa uchumi

Mwadzaya, Thelma1 Oktoba 2008

Bunge la Senate nchini Marekani limeafikiana kuupigia kura tena mswada unaolenga kuokoa soko la fedha.

https://p.dw.com/p/FS03
Kiongozi wa chama kilicho na uwakilishi mkubwa kwenye Bunge la Senate Seneta Harry ReidPicha: AP


Mpango huo unazimia kutumia dola bilioni mia saba kuiwezesha serikali kununua taasisi za fedha zinazokabiliwa na matatizo ya fedha.Kwa mujibu wa Kiongozi wa chama kilicho na uwakilishi mkubwa katika Bunge la Senate Harry Reid hatua hiyo imeungwa mkono na bunge hilo kwa minajili ya kuokoa uchumi wa Marekani.Rais George Bush kwa upande wake amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za dharura.


Rais Bush alisisitiza kuwa lengo la hatua hiyo ni kulinda maisha ya raia wa Marekani.Hapo jana Baraza la wawakilishi la Marekani lilipinga mswada wa kuidhinisha dola bilioni mia saba kwa lengo la kuokoa jahazi la uchumi wa nchi hiyo.Mswada huo ulipingwa zaidi na wabunge wa chama cha Republikan.Bunge la Marekani Congress lilifungwa hapo jana kwasababu ya sherehe za mwaka mpya wa Kiyahudi Rosh Hashanah.