1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BURHAKABA, SOMALIA.hali ya wasiwasi yazidi

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCji

Wapiganaji wanaounga mkono mahakama za waislamu nchini Somalia na wanajeshi watiifu kwa serikali ya mpito leo wamejiweka katika hali ya tahadhari huku wakiendelea kuchimba mitaro katika pande mbili za msatri wa mbele katika nchi hiyo ya upembe wa Afrika inayokabiliwa na hatari ya kuzuka tena vita.

Wakati huo huo Ethiopia imekemea onyo lililotolewa na muungano wa mahakama za kiislamu kwamba haitasita kuivamia serikali ya mpito ya Somalia iwapo Addis Ababa haitawaondoa wanajeshi wake kutoka mji wa Baidoa katika kipindi cha wiki moja.

Hali ya wasiwasi imeikumba nchi ya Somalia tangu baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kupelekwa wanajeshi wa kulinda amani nchini humo kuisaidia seikali ya mpito.