1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ucahguzi wa bunge na madiwani haukuwa wa haki na huru

Admin.WagnerD3 Julai 2015

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wamesema uchaguzi wa bunge na madiwani uliofanyika siku ya Jumatatu nchini Burundi, haukuwa huru na wa haki.

https://p.dw.com/p/1FsAf
Parlamentswahlen in Burundi Wahllokal Wahlhelfer Wahlbeteiligung
Uchaguzi wa bunge na madiwani nchini BurundiPicha: Getty Images/AFP/P. Moore

Uchaguzi huo uliogubikwa na vurugu na kususiwa na baadhi ya vyama vya upinzani ulifanyika licha ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuitolea mwito serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi huo kufuatia hali mbaya ya kiusalama. Hata hivyo hadi leo raia wa nchi hiyo wanaendelea kusubiria kwa hamu kubwa matokeo hayo yaliokuwa yatolewe rasmi hapo jana. Kwa mengi zaidi juu ya hilo, Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu Amida Issa aliyeko mjini Bujumbura .

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri:Yusuf Saumu