1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush aendelea na ziara yake Tanzania

18 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D9Cl

Rais George W Bush wa Marekani amewasili leo katika mji wa Arusha ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake nchini Tanzania.

Rais Bush amezindua mpango mpya wa kusambaza vyandarua maalum kumlinda kila mtoto mtanzania mwenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka mitano kutokana na mbu wanaosababisha ugonjwa hatari wa malaria.

Baada ya kuitembelea hospitali ya wilaya ya Meru mjini Arusha, rais Bush amesema vyandarua vya kuzuia mbu ni mojawapo ya teknolojia rahisi lakini inayofaa kuleta matokeo yanayotarajiwa.

Rais Bush pia amezungumzia kuhusu msaada wa Marekani kwa fuko la fedha la kimataifa la kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria, akigusia kampeni za kunyunyiza dawa za kuua wadudu, kuwatibu watoto na akina mama wajawazito na kusambaza vyandarua vilivyonyunyiziwa dawa ya kuua mbu.

Tanzania ni kituo cha pili cha ziara ya siku sita ya rais Bush barani Afrika iliyoanza nchini Benin Jumamosi iliyopita.

Rais Bush atazitembelea pia Rwanda, Ghana na Liberia kabla kurejea mjini Washington.