1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush ahutubia taifa na kujadilia masuala mbalimbali

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzLo

WASHINGTON:

Rais wa Marekani George W.Bush ametetea jinsi alivyoshughulikia vita nchini Iraq,akitilia mkazo kuwa hali ya kuongezea wanajeshi zaidi nchini humo imeleta ahueni kidogo.Bush amelihimiza baraza la Congress,kulifadhili kikamilifi , jeshi la Marekani lilioko Iraq na Afghanistan akitoa hoja kuwa vikosi vya ziada vimesaidia kupunguza ghasia na kuwezesha kupatikana hatua ya kisaisa kuchukuliwa na serikali ya Iraq.

Katika hotuba yake hiyo kwa taifa ya kila mwaka ,Bush pia amesema kuwa juhudu za kidiplomasia kukomesha mzozo kati ya Israel na Palestina,ni sehemu ya mkakati ya wa vita Marekani inavyopigana dhidi ya ugaidi.Aidha ameahidi kushirikiana na jamii ya kimataifa kuizuia Iran kutopata uwezo wa kutengeneza silaha za Nuklia. Kuhusu masuala ya ndani ya Marekani,Bush amewaomba wabunge kupasisha haraka mpango wa mda mfupi, wa kuupiga jeki uchumi ,mpango unaogharimu dola billioni 150.Amesema hatua hii itasaidia kuepuka kudorora kwa uchumi.

Na katika tukio jingine,Mbunge maarufu wa baraza la senate la Marekani-Ted Kennedy amembariki Baraka Obama kuwania urais wa Marekani kwa kutumia tiketi ya chama cha Democratic Party. Kennedy amesema kuwa amevutwa na tabia ya Obama na kuhisi kuna mabadiliko fulani yanayotarajiwa.Baadae ,Obama na Seneta Kennedy walikaa pamoja wakati wa hotuba ya rais Bush kwa taifa.