1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush atangaza kwenda Afrika mwakani kutathmini misaada ya ukimwi

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVPQ

NEW YORK.Leo ni siku ya UKIMWI duniani, ambapo Umoja wa Mataifa uliitangaza siku hii katika kushadihisha mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI.

Nchini Marekani Rais George Bush amewapongeza wote waliyo katika mapambano dhidi ya maradhi hayo, na kusema kuwa kutokana na kuwajibika kwao, mamilioni ya watu waliyoona maradhi hayo kama ni hukumu ya kifo, sasa wana matumaini mapya.

Rais Bush ambaye alitangaza kuwa atafanya ziara ya afrika mapema mwakani, alisema kuwa Marekani itaendelea kutoa msaada wake katika vita hiyo.