1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush aunga mkono Ukraine na Georgia kujiunga na NATO.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYaE

Kiev.

Rais wa Marekani George W. Bush ameahidi kuunga mkono nia ya Ukraine na Georgia kujiunga na jumuiya ya NATO licha ya upinzani wa Urusi.

Baadhi ya wanachama wa umoja huo wa mataifa ya Ulaya pia wanapinga kuipanua jumuiya hiyo kuelekea upande wa mashariki.

akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na rais wa Ukraine Viktor Yushchenko mjini Kiev, Bush amesema kuwa anatoa mbinyo kwa washirika wake wa mataifa ya magharibi katika mkutano wa wiki hii wa NATO nchini Romania kuunga mipango hiyo ya uanachama wa Ukraine na Georgia.