1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush na Karzai wakamilisha mazungumzo yao ya siku mbili

7 Agosti 2007

Marais wa Marekani na Afghanistan wasema Ng'o hakuna ridhaa kwa kundi la Taliban

https://p.dw.com/p/CB29
MaraisGeorge Bush na Hamid Karzai
MaraisGeorge Bush na Hamid KarzaiPicha: AP

Marais George W. Bush wa Marekani na Hamid Karzai wa Afghanistan wameapa kuliangamiza kundi la Taliban ambalo rais Karzai amelitaja kuwa sio tishio kwa serikali yake.

Rais Karzai aliyasema hayo wakati alipokutana na rais Bush katika eneo la Camp David karibu na mji wa Washington nchini Marekani.

Viongozi hao pia wamekubaliana juu ya kutotolewa ridhaa ya aina yoyote kwa kundi la Taliban linalowashikilia mateka 21 raia wa Korea Kusini.