1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUsh-Vita nchini Irak havishindiki

21 Desemba 2006

Wahariri wa magazeti ya ujerumani leo wametuwama juu ya mada ":kuungama kwa rais Bush kwamba Marekani haishindi wala haitashindwa Irak na jinsi rais wa Ujerumani H.Köhler anavyoongoza:

https://p.dw.com/p/CHU9

Katika gazeti la Westfälischen Anzeiger linalotoka Hamm tunasoma kuwa, masaa 48 tu baada ya kumtawaza waziri wake mpya wa ulinzi-Gates- rais George Bush aliwasangaza watu kwa njia ambayo hakuna alietazamia:Aliungama kwamba vita nchini Irak haviwezekani tena kuleta ushindi.

Kuutambua ukweli huo angeweza pia Bush kujua kabla kuanza kuuhujumu mji mkuu wa Iraq Baghdad,alipoanzisha vita-lasema gazeti.

Sasa Bush amechelewa kutanabahi kuwa ametumbukia katika janga kubwa la siasa za nje,amepoteza mabilioni ya fedha bure na kutoa mhanga maisha ya hadi askari 3.000 wa kimarekani.

Gazeti la OBERMAIN-TAGBLATT linatufanywe tuwaze linapoandika:

“Mpendavita George Bush hataki kuona ukweli kwamba nguvu zake kubwa za kijeshi, zinasimamia nguzo yenye kuregarega kila mizozo duniani inapoongezeka.

Aliomba kuidhinishiwa dala nusu-bilioni hapo 2001 ili kugharimia vita nchini Irak na Afghanistan. Laiti angelitumia akiba hiyo kupambana na shida na dhila nchini Irak,pasingeibuka wahanga wengi wakujiripua mabomu kwavile, hawakuona matumaini ya maisha bora duniani.

Gazeti linalotoka erfurt-THÜRINGER ALLGEMEINE linasema:

„Tangu awali ilikua dhahiri-shahiri:ikiwa Marekani yataka kubadili mkondo wa mambo nchini Irak,hainge badili na George Bush.Lakini, baada ya kushindwa chama chake katika uchaguzi wa Bunge ,Bush alibidi kuridhia shingo upande mapendekezo ya Tume ya Baker.

Mapendekezo ya Tume hiyo kuwa, vikosi vya Marekani vipunguzwe nchini Irak na wairaki wenyewe wabebe jukumu kubwa zaidi la usalama wao,sasa hayafuati Bush na anafanya kinyume chake.“-Ni maoni ya THÜRINGER ALLGEMEINE.

Hata gazeti la Heidelberg-RHEIN-ZEITUNg linaona kuongeza zaidi askari wa kimarekani nchini Irak hakusaidii kitu.Laandika:

„Kwamba hata mwenyewe George Bush sasa anazungumza kwamba Marekani haishindi vita nchini Irak,si muhimu sana .Maamirijeshi wake wanasema hivi sasa tena hadharani kwamba, Bush amelikongoa mbawa jeshi bora kabisa duniani huko Irak.Na hii ndio sababu sasa ana azma ya kuongeza askari kulipa nguvu mpya .

Lakini hakuna ishara zinazobainisha kwamba katika vita vya sasa vya kuuma na kupuliza nchini Irak ambamo Marekani katika safu zote inajikuta katika vita vya kienyeji,kuna kitakacho badilika.

Likitugeuzia mada, gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz, linazungumzia mtindo war ais Horst Köhler wa Ujerumani wa kuongoza wadhifa wake wa urais:mtindo huo ukitazamiwa kukodolewa macho zaidi mara hii katika mkutano wake wa desturi na Kanzela Angela Merkel.

Gazeti laandika:

„Horst Köhler ni mtu mwenye mawazo yake ya kipekee na hili sio jambo linalomjia baadhi ya nyakati tu.Na tabia hii yawezekana ameitambua kanzela Angela Merkel…Rais Köhler anashughulikia mno siku za usoni za taifa hili.Anaelewa kwamba Ujerumani kutokana na kustawi sasa kwa uchumi, hii haitatatua matazizo yake ya kimsingi.

Ni misingi ya kijamii ambayo imeizonga nchi hii.Na ndio maana amezindua pafanyanyike mageuzi zaidi ,kwani rais wa Ujerumani sio tu anashika nafasi ya kwanza katika dola, bali pia ni mkosoaji mkubwa na barabara.“