1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush yaihakikishia ulinzi Israel

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cn7H

JERUSALEM:

Rais George Bush wa Marekani ambae amewasili Israel katika ziara yake ya kwanza nchini humo tangu achukue hatamu nchini mwake,akiwa Tel Aviv amesema kuwa Isreal na Marekani ni washirika wakubwa.

Kiongozi huyo amepangiwa kwenda Ramallah katika eneo linalokaliwa la West Bank.Atakutana kwa mazungumzo na rais wa Palestina Mahmood Abbas. Tayari amekutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Jerusalem.

Bush amelaumiwa kwa kupuuza mgogoro wa mashariki ya kati wakati wa uongozi wake wa miaka saba.

Katika eneo la Gaza watu wapatao 200 waliandamana wakimhimiza Bush aache kuipendelea Israel.