1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO : Kujizatiti kwa Rice kwaishajiisha Misri

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FA

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amerudi tena nchini Israel kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa viongozi wa amani ya Mashariki ya Kati.

Rice hapo jana ameweza kuungwa mkono kwa tahadhari na Misri kwa ajili ya mkutano huo wa amani kati ya Israel na Wapalestina uliopangwa kufanyika nchini Marekani hapo mwezi wa Novemba.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Ahmed Aboul Gheit amesema kujizatiti kwa Rice katika kufikia ufumbuzi wa mzozo huo ni jambo lenye kushajiisha.

Wachambuzi wa mambo wanasema uungaji mkono wa Misri ambayo imekuwa ikisita sita huko juu ya uwezekano wa kufanikiwa kwa mkutano huo utarahisisha ulimwengu wa Kiraabu kuunga mkono.