1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Marekani tayari kukutana na Iran kuhusu Iraq

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2R

Makamu wa Rais wa Marekani, Dick Cheney, amesema kwamba Marekani iko tayari kushauriana na Iran kuhusu hali nchini Iraq.

Msemaji wa makamu huyo wa rais, Bi Lea Anne McBride amewaambia waandishi wa habari mashauriano kati ya nchi hizo mbili yatakuwa kuhusu masuala ya Iraq peke yake.

Msemaji huyo alisema hayo baada ya wizara ya mambo ya nje ya Iran kutangaza imekubali maombi rasmi ya Marekani ya kuwa na mikutano nchini Iraq hivi karibuni kuzungumzia usalama.

Makamu wa rais wa Marekani yumo katika mkondo wa mwisho wa ziara yake katika Mashariki ya Kati.