1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Mkutano wamalizika kwa tofauti ya mawazo.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4h

Mkutano wa siku mbili wa kimataifa ulioitishwa kuimarisha hali ya mambo nchini Iraq umemalizika nchini Misr kukiwa na mawazo tofauti miongoni mwa wanadiplomasia.

Marekani imesema kuwa imeridhishwa baada ya maafisa wa nchi hiyo kufanya mazungumzo ya pembezoni mwa mkutano huo na wenzao wa Syria na Iran, mataifa mawili jirani ya Iraq.

Katika mkutano huo katika mji wa kitalii wa Sham el-Sheikh , waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Manouchehr Mottaki , amezilaumu sana sera za Marekani nchini Iraq, akilaumu kuhusu miaka minne ya kuwapo majeshi ya Marekani kwa kuendeleza ghasia za kimadhehebu.

Mazungumzo hayo siku ya Alhamis yalisababisha ahadi ya dola bilioni 30 kama msaada kwa kupunguza madeni kwa Iraq.

Mjini Baghdad msemaji wa kundi la Wasunni ameilaumu serikali ya Iraq inayoongozwa na Washia kwa kushindwa kuiunganisha nchi hiyo.