1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Mwito kuahirisha mkutano wa amani

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FI

Waziri wa Nje wa Marekani,Condoleezza Rice amewasili Misri kujadiliana na Rais Hosni Mubarak juu ya mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati uliopangwa kufanywa mwezi Novemba.Lakini sauti zinazidi kupazwa hasa nchini Misri na Saudi Arabia zikitaka mkutano huo uahirishwe,kwa hofu kuwa juhudi za kutafuta amani katika eneo hilo zitaathirika vibaya,ikiwa mkutano huo wa kilele hautofanikiwa.Misri inashikilia kuwa mkutano huo uahirishwe ili kupata nafasi zaidi kuondosha tofauti za maoni zilizokuwepo.

Kabla ya kwenda Misri,Rice alikutana na Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas katika Ukingo wa Magharibi.Akasema,kuundwa kwa taifa la Palestina ni miongoni mwa vipaumbele vya juu vya Marekani.