1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Watuhumiwa kadha wakamatwa wakipanga njama za mashambulizi.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmP

Polisi wa Misr wamewakamata watu 11 rais wa mataifa ya Ulaya , Marekani na wengine kadha kutoka mataifa mengine ya Kiarabu.

Wizara ya mambo ya ndani ya Misr imeliita kundi hilo mtandao wa Kiarabu wa mataifa ya magharibi ambalo lilikuwa linapanga mashambulizi ya kigaidi katika mataifa kadha ya mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na Iraq.

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa watu hao walikuwa wanawaandikisha watu wengine , wakiwahimiza kutekeleza vita vya Jihad.

Watuhumiwa hao walikamatwa wiki iliyopita na walikuwa wakiishi nchini Misr wakijidai wanajifunza lugha ya Kiarabu pamoja na Uislamu.