1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo.Abbas kuelekea Gaza kwa mazungumzo na waziri mkuu Ismail Haniya.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvQ

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Palestina Mahmud Zahar ameyatolea mwito mataifa ya Kiarabu yaingilie kati haraka kukomesha mashambulio ya Israel huko ukanda wa Gaza.

Waziri huyo wa kutoka chama cha Hamas amesema nchi za Kiarabu zinabidi ziwajibike mbele ya Wapalestina na kuingilia kati haraka kupitia mashirika ya kimataifa na kupitia kila hali ili kumaliza mashambulio ya Israel.

Zahar anaefanya ziara ya siku kumi nchini Misri, amekuwa na mazungumzo na kiongozi wa udugu wa Kiislamu Mohamed Mehdi Akif.

Wakati huo huo kiongozi wa utawala wa ndani wa Palestina Mahmoud Abbas anatazamiwa kwenda Gaza hii leo kwa mazungumzo pamoja na waziri Mkuu Ismail Haniye na viongozi wa makundi mengine ya kisiasa.

Ziara hiyo inatokea katika wakati ambapo mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano wa kitaifa yanaashiria kuleta tija.