1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Rais wa zamani wa Iraq afariki Jordan

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWW

Rais wa zamani wa Iraq Abdul-Rahman Aref amefariki katika mji mkuu wa Jordan wa Amman.Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Pan arab al Arabiya.Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu kifo chake.Marehemu Aref alikuwa mwanasiasa na mwanajeshi aliyekuwa madarakani nchini Iraq kuanzia Aprili 16 mwaka 66 hadi Julai 17 mwaka 68.