1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAMP DAVID: Rais Bush akutana na Brown

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdj

Rais George W Bush wa Marekani atafanya mazungumzo ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown hii leo huko Camp David.

Gordon Brown anajaribu kutafuta uugwaji mkono kuhusu mpango wa amani katika jimbo linalokabiliwa na mzozo la Darfur nchini Sudan na mazungumzo ya kibiashara ya shirika la kibisshara duniani, WTO, yaliyokwama.

Mazungumzo baina ya rais Bush na Gordon Brown yatakayohudhuriwa pia na mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani na Uingereza, yanatarajiwa kugubikwa na tatizo la Irak.

Kabla kuwasili kwenye kambi ya jeshi ya Andrews nje ya mji wa Washington, bwana Gordon Brown alirudia tena kwamba anataka kuiepusha mbali serikali yake na Marekani kwa sababu ya ukosoaji kuhusiana na swala la Irak.