1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Canada kuondosha vikosi vyake Afghanistan

7 Novemba 2009

Canada imesema itawarejesha nyumbani wanajeshi wake, kutoka Afghanistan.

https://p.dw.com/p/KQTF
Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper.Picha: AP

Canada inajitayarisha kuviondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan. Kuambatana na uamuzi uliopitishwa na bunge la nchi hiyo,wanajeshi wake watakuwa wamerejea nyumbani ifikapo mwisho wa mwaka 2011. Msemaji wa kijeshi amesema, mkuu wa majeshi ametoa amri ya kuanza kuwarejesha nyumbani wanajeshi 2,800 walioko kusini ya Afghanistan.

Waziri Mkuu wa Kanada Stephen Harper ameeleza waziwazi kuwa yeye hatorefusha muda wa vikosi vyake nchini Afghanistan hata akiombwa na Rais wa Marekani Barack Obama.Tangu mwaka 2002, Kanada imepoteza wanajeshi 133 na mwanadiplomasia mmoja nchini Afghanistan.